VIPENGELE VYA UDEREVA VYA KUJIHAMI.
Ili kutekeleza kanuni ya kuzuia ajali, Dereva yeyote anatakiwa
kuelewa vizuri mambo ya msingi yafuatayo;-
1. Kujua
2. Kuwa macho
3. Kuangalia mbele
4. Kuamua
5. Ujuzi wa kugundua , hatari kwa haraka
KUJUA
Dereva anapaswa kuelewa michoro na alama za barabarani.
i. Alama za barabarani na michoro inawakilisha
lugha, ambayo kila mtumiaji wa barabara anatakiwa kuijua vizuri, kuiheshimu na
kuitafasiri kama inavyotakiwa.
ii. Kwa bahati nzuri inawakilishwa na
vbitambulisho vya vikundi vikuu vitatu
a. Rangi Nyekundu, Nyeusi, Njano, Nyeupe, bluu,
kijani.
b. Umbile Mviringo, Pembe tatu, Pembe nne na
pembe tano.
c. Alama – Maandishi, Picha na Michoro.
iii. Alama na michoro ya barabarani ni lazima ziwe
na sifa zifuatazo.
a. Zilenge kuongeza ufanisi wa mtandao wa
barabara.
b. Zitoe ujumbe ambao ni wazi unaoeleweka
kirahisi kwa kila mtumiaji wa Barabara.
c. Zizingatie sheria za usalama
barabarani za kitaifa na kimataifa
d. Ziwe na muundo wa alama moja kitaifa
unaolingana na makubaliano ya umoja wa kimataifa kwa alama za msingi.
e. Ziwekwe sehemu ambazo ni lazima kuwepo, ili
zitoe ujumbe sahii kwa watumia Barabara,
f. Ziwekwe umbali unaotakiwa kutoka sehemu husika
g. Zifanyiwe matengenezo ya marakwa mara.
Mambo ya msingi ya kujiuliza kwanza
a. Alama ni kiashirio kinachomuongoza mtu kwenye
mambo na kumfanya afanye mambo vizuri.
b. Alama za barabara ni uongozi uliowekwa
kisheria kutoa muongozo wa kisheria ili kumuwezesha
dereva aweze kufanya kazi zake kirahisi na kwa
ufanisi ili kwamba atumiapo barabara aweze kwenda kwa
uysalama zaidi bila kupata au kusababisha ajali.
c. Alama za barabarani ni kitu ambacho
hakitarajiwi kutokuweko
d. Wataalamu waliamua kukaa na kutunga alama za
usalama barabarani alama hizo zimegawanyika katika makundi makuu
matano
· Alama za Amri
· Alama za Onyo
· Alama za taarifa
· Alama za maelekezo
· Alama za michoro chini ya barabara , taa za
kuongoza watumiaji wa barabara.
Alama za Amri
Alama hizi zimegawanyika katika makundi makuu matatu yafuatayo;-
- Amri za kukataza.
- Amri za kulazimisha au kuruhusu.
- Amriza kutoa kipaumbele
Amri za kukataza ;-
Alama hizi zina waonyesha watumiaji wa barabara sehenu ya
barabara iliyokatazwa au mwisho wa sehemu iliyokatazwa kufanya jambo
Fulani kama itakavyoonyeshwa kwenye alama yenyewe alama
hizi ni halali
· Katika mwelekeo wa kawaida wa wanaotumia
barabara
· Kutoka sehemu iliyopo hadi njia panda iliyo
karibu na alama husika .
Alama za amri ya kukataza zina umbo la mviringo, mpaka mwekundu
na picha au mchoro wenye rangi nyeusi, nyekundu au bluu katika madhari
Alama au amri ya kukataza zinawekwa karibu sana na sehemu
husika
Alama za kulazimisha au kuruhusu
Ø Hizi
ni alma zinazzotumika kwa watumia barabara kuelekea mwelekeo au njia
Fulani kati ya nyingi zilizopo kwenye njia panda , pia alama hizi
zinatumika kuwaongoza wanaotembea kwa miguu na wapanda baiskeli kwenye njia
moja kati ya njia zilizopo kwenye eneo husika
Ø Amriza
kulazimisha zina umbo la mviringo mpaka mdogo mweupe na picha ai mchoro mweupe
katika madhari nyuma bluu alama hizi zinawekwa karibu sana na njia panda
Ø Alama
za kipaumbele na kupisha njia panda ni sehemu yenye migogoro mingi kati ya
watumia barabara kuliko sehemu nyingine yoyote ile barabarani. Ili kurekebisha
migogoro hiyo kati ya watumia barabara. Sheria ya Usalama barabarani inatumika
(toa kipaumbele kwa madereva wa magari wanaokaribia njia panda
kutoka kulia ) lakini sehemu yenye magari mengi ambapo madereva
hawawezi kutathimini vizuri hatari iliyopo basi sehemu hiyo njia panda sheria
ya usalama barabarani haitatumika tena badala yake zitatumika alama
za kipaumbele
Ø Alama
hizi zina maumbo mbali mbali kulingana na ujumbe au amri inayokusudiwa katika
alama husika.
Alama za tahadhari au Onyo
Ø Alama
hizi zinawaonya madereva na watumia barabara wengine juu yaq hatari iliyopo au
inayoweza kuwepo mbele yao
Ø Alama
hizi zinawqekwa upande wa kushoto wa barabara kati ya mita mia
hadi mia mbili (100-200m) toka sehemu yenye hatari
Ø Sehemu
zenye njia panda nyingi hasa mjini umbali huo hupungua hadi mita
hamisini (50m)
Ø Sehemu
ya barabara yenye alama hizi dereva anatakiwa kupunguza kasi ya gari lake.
Ø Alama
za tahadhariu au onyo zina umbo la pembe tatu lenye kitako pembe mbili chini,
mpaka mwekundu na picha au mchoro wa hatari iliyopo au inayoweza kutokea mbele
katika mandhari ya nyuma nyeupe.
Alama za Taarifa
Ø Alama
za taarifa huwataarifu madereva na watrumia barabra wengine juu ya barabara ,
sehemu muhimu na sehemu senye huduma mbalimbali ambazo ni muhimu kwao , kati ya
alama hiziz zipo pia zenye uhusiano na sheria ya usalama barabarani
ambazo zinatoa masharti Fulani ambayo mtumiaji wa barabara akiamua
kutumia sharti afuate sheria na si vinginevyo Kwa Tanzania ni hiari
ya dereva kutumia barabara hiyo ,lakini akiamua ni lazima aendeshe gari lake
uelekeo ulioonyeshwa kwenye alama hiyo.
Ø Alama
za maeneo ya huduma, hizi ni taa ni alama zinazowafahamisha madereva na watumia
barabara wengine juu ya huduma mbalimbali wanazoeweza kupata katika maeneo
husika
Ø Alama
hizi zina umbo la pembe mraba nne, ulingo wa Bluu picha nyausi au nyekundu
katika madhari nyeupe nyuma
Alama za maelekezo
Ø Hizi
ni alama za kuwafahamisha madereva wa magari sehemu maalumu nba muhimu
Ø Alama
hizi zina umbo la pembe nne Mstatili au mraba ulingo wa bluu picha nyeupe au
nyeusi madharri ya bluu au kijani nyuma.
Ø Alama
hizi zinawekwa kabla ya njia panda au kwenye njia
panda ili kuwasaidia madereva na watumiaji wengine wa
barabara kuchagua barabara zinazofaa kuwafikisha waendako
na kuwaongoza kwenye mtanadao wa barabara kupita na hata kuzunguka kwenye
maeneo ya makazi ya watu
Alama za michoro ya chini ya barabara na taa za barabarani
Ø Michoro
ya barabarani ni ni mmichoro iliyochorwa kwa lengo la kurekebisha
msongamano wa magari pamoja na kuwaonya au kuwaongoza watumiaji wa barabara
Ø Michoro
hiyo ya barabarani imegawanyika katika makundi makuu yafuatayo;-
Mistari ya Onyo
Mistari ya kukataza
Mistari inayogawa njia katikati ya
barabara ya magari
Mistari inayogawa barabara
Mistari inayogawa njia ya magari ya
abiria katika barabara
Mistari ya kutokea pembeni mwa
barabara ya magari
Mistari ya kipaumbele
Mistari ya kusimama
Mistari hii pia huchoirwa karibiu na njia
panda sehemu ya barabara hii dereva hatakiwi kuvuka njia kwa sababu
ya hatari iliyopo ikiwa atavuka basi avuke kwa tahadhari kubwa
Taa za kuongoza watumia barabara
Ø Taa
hizi zinalenga kuondoa migogoro kati ya watumia
barabara kwenye njia panda au barabara zenye matumizi makubwa
Ø Taa
nyekundu humaanisha usiingie njia panda simama
Ø Nyekundu
na njano usiiingie nja panda simama
Ø Njano
usiingie kwenye njia poanda simama
Ø Kijani
ingia kwenye njia panda endapo ni salama.
LIJUE GARI LAKO.
Mfumo wagea Gea za Gari za aina mbali mbalizenye kutumia mfumo
wa Manyo ( Manual)
Mfumo wa gea za
kukanyaga katika magari manyo
CLUTCH ; Kazi
yake ni kuondoa gari na kutenganisha Engine na Gearbox.
BRAKE ; Kazi
yake ni kupunguza mwendo na kusimamisha gari
ACCELERATOR;
Kazi yake ni kuongeza mwendo kasi wa gari na muungurumo na inapoachiwa kidogo
mwendo hupungua, inaongeza kasi ya uhcomwaji wa mafuta.
Ni Muhimu Kukumbuka kuwa Unapotaka kusimama unatakiwaq kukanyaga
Clutch na Brake kwa pamoja ili gari lisizime linaposimama.
Kazi ya gea namba moja Ni kuondoa gari na kupanda mlima
mkali na wakati wa kuteremka mlima mkali
Kazi ya gea namba mbili Ni kuifanya gari kuwa nyepesi zaidi na
kuongeza mwendo
Kazi ya gea namba tatu na nne Ni kufanya gari kuendelea kuwa
jepesi zaidi na kuongeza mwendo
Namna ya kupanga gea kutoka gea nzito kwenda gea nyepesi;
Kutoka 0-10 MPH
Gea . No 1
Kutoka 10-20 MPH.
Gea . No 2
Kutoka 20-30 MPH.
Gea. No 3
Kutoka 30-40 MPH.
Gea. No 4
Kutoka 40-50 MPH
Gea. No 5
Kutoka 50-120 MPH. Mwendo
utaendelea kuzaliswa na gia No 1 & 2
Jinsi ya kupangua gea kubwa kwenda gia ndogo
Kama gari lilikuwa linatembea kiasi cha mwendo upatao
60MPh itakubidi upunguze mwendo hadi 50MPH au 40MPh ndipo uingize gia nambari
nne
Endapo inatembea mwendo kiasi 40 MPH itakubidi upunguze mwendo
hadi kufikia 30MPH ndipo uingize gia nambari tatu
Kama gari ilikuwa inatembea kiasi cha mwendo upatao 30MPH
itakubidi upunguze mwendo hadi kufikia 20MPH ndipo uingize gea nambari mbili
DASH BOARD
Dash board ni chombo ambacho kinamjulisha na kumwezesha dereva
kugundua hitilafu zinazoweza kujitokeza anapoendesha gari barabarani kwa mfano
· Kusoma speedmeter – hiki ni chombo
ambacho hupima kasi au mwendo wa gari
· Mail gauge – hiki ni chomboambacho hupima au
kuhesabu au kurekodi ni mwendo au umbali gani gari limetembea
· Fuel gauge – ni kipimo cha kuonyesha ni kiasi
gani cha mafuta aidha Petrol au diesel iliyoko kwenye tank la gari
· Oil gauge – ni kipimo chenye kufanya kazi ya
kuonyesha ni kiasi gani cha oil kimebakia kwenye injini
· Water temperature gauge ni kipimo ambacho
kinaonyesha joto la injini limepanda kiasi gani na pia kuonyesha
maji yamepata moto kiasi ghani kwenye radiator
· Alternator gauge au alternator charge hiki ni
chombo cha kuonyesha kuwa kifua umeme katika gari hakifanyi kazi kwa msingi huo
maana yake ni kuwa haichaji na hivyo maana yake ni kuwa umeme haufuliwi
· Right indicator – ni taa maalumu yenye mlio
Fulani kuashiria kuwa unakusudia kukata kwenda upande wa kulia
· Left indicator – ni taa maalumu yenye mlio
Fulani kuashiria kuwa unakusudia kukata kwenda kushoto
Dash Board kama
inavyoonekana katika mchoro chini.
Katika Dash Board kunakuwa na maswala kadhaa
yanayoweza kusoma mambo kadhaa yafuatayo
0 2 6 8 6 4 2
|
Water temp
|
Brake Light
|
Alternator
|
Fuel gauge
|
Right
|
Left indicator
|
Fuel
|
UTUNZAJI WA GARI
Katika utunzaji wa gari kwa ujumla tunazungumzia ukaguzi wa
gari.Ukitaka gari lako liwe katika hali nzuri kila ulitumiapo/kuwa na uhakika
wa usalama wako na wa gari lako liwapo barabarani, ni muhimu sana kulikagua
hari kila siku asubuhi kabala ya kuliendesha na pia kuwa na utaratibu wa
kulifanyia service kila linapotembea kilomita kadhaa.
Ukaguzi wa gari
1. Kitu cha kwanza kabisa ni kulikagua gari lako
kwa nje, utafanya ukagfuzi wa matairi kwa kuangalia
· Upepo na nati kama zimelegea au la
· Kashata za Matairi kama hazijaisha yaani ziko
kipara
Kisha utafungua Bonet na hapa utaangalia
· Maji kwenye rejeta (radiator) kama yapo
· Oil kwenye injini kwa kutumia deep stick
- Hakikisha unapopima oil gari liko katika tambarare
ili uweze kupata level halali ya oil
- Oil inayotumika kwenye injini kwa kawaida ni
nambari 40
- Deef oil nambari 140
- Gear box ni oil nambari 90
· Mafuta ya Brake (Brake fluid) na clutch
· Maji ya betrii, yaani unafungua betrii na
kuangalia kama
- Maji yamepungua unaongeza maji baridi
Distrilled water
- Kama ni jipya umemwaga maji yote na kuweka
Acid maarufu kama maji makali HCI
- Maji yakiisha ndani ya betrii , batrii itakufa
baada ya hapo
- Unafunga tena bonet.
2. Sasa unaingia ndani ya gari na unaaangalia
· Kaa kwenye kiti chako na hakikisha
kimekaa sawasawa
· Kagua pedle zote kama zinafanya
kazi sawasawa yaani hapa tunazungumzia
- Brake kama iko sawa na inafanya kazi
- Clutch kama iko sawa na inafanya kazi
- Acceletator kama iko sawa na inafanya kazi.
· Kagua dashboard kama taa zote za vitu vyote
zinafanya kazi vema yaani
- Water temperature gauge
- Alitanatory charge
- Oil gauge
- Fuel gauge
- Mail gauge .n.k.
· Waipa kama zinafanya kazi vema
· Hand brake kama inafanya kazi vema
· Usukani kama umekaa vema
· Mkanda
· Taa zite kama zinafanya kazi Hususani
indicator
· Wema side mirror vema kukuwezesha
kuona chochote kwa nyuma au pembeni
· Kioo cha kuangalia magari nyuma pia kiwekwe
kukuwezesha kuona
Ukimaliza yote hayo sasa uko huru au salama kuendesha gari lako.
KUONDOA AU KUENDESHA GARI.
Unapokuwa umekagua gari lako na kulikuta liko katika hali nzuri
sasa unataka kuliendesha na kuanza safari na gari lako, unapoingia kwenye gari
na kuikuta iko katika gea namba moja basi sasa unapaswa kufanya maswala
yafuatayo.
i. Weka switch/ yaani ufunguo wa gari katika
sehemu yake
ii. Kanyaga clutch mpaka mwisho
iii. Ondoa gea namba moja na kuliweka gari huru
yaani free
iv. Ondoa mguu kwenye clutch
v. Anza kuwasha ufunguo wa gari Satrt/Switch gari
vi. Sikiliza muungurumo kidogo
vii. Kanyaga clutch mpaka mwisho/pamoja na brake
kulisaidia gari lisiweze kurudi nyuma
viii. Ondoa gari kutoka kwenye free mpaka kwenye
nambari moja gea hii mara nyingi hujulikana kama gea ya kuondokea
ix. Legeza mguu wa kwenye clutch mpaka unasikia
gari kama inaondoka hivi mlio unakuwa umebadilika na unakuwa constant
x. Kumbuka kutoa handbrake
xi. Ongeza mafuta kidogo na na kulegeza clutch na
gari litaanza kuondoka na linapoondoka achia clutch, lakini usiachie
ghafla, taratibu baada ya kuona baada ya kuona gari liko kwenye mwendo wa
kawaida
xii. Lipe gari nguvu kwa kuongeza mafuta na
badilisha gea nambari moja kwenda nambari mbili, unapobadilisha gea
hakikisha kuwa unaachioa accelerator na kukanyaga clutch na baada ya
gea kuingia unaachoia clutch na unakanyaga acceleretaor
xiii. Utaendelea na safari kwa kubadilisha gea
nambari mbili mpaka tatu na kuendelea
Kumbuka gea nambari moja sio ya kutembelea hivyo usiiache kwa
muda mrefu bila ya kuibadilisha
Unapoendesha gari hakikisha kuwa una vyeti vyako ili isiwe kero
kwa traffic vyeti hivyo ni
a. Leseni ya kuendeshea driving Licence –
hakikisha haijaisha na pia iwe ni daraja linalohusika
b. Kadi ya njia (T.L.B)
c. Kadi ya gari ambayo kwa kawaida huwa na
o Jina la gari
o Namba ya gari
o Jina lako
o Gari lilitengenezwa wapi
o Limesajiliwa lini hapa nchini
o Engine namber
o Chases Nuimber n.k.
Vitu muhimu kuwa navyo unapoendesha gari ni pamoja na
· Spare tyre-tairi la akiba
· Jeki
· Na spana ya kuondoa tairi Wheel spanner
Safari ya mbali
· Kisanduku cha huduma ya kwanza chenya panadol,
aspirin, spirit, iodine, bendeji, pamba, plaster, wembe mkasi, pini n,k.
· Spana za dharula
· Plaizi na Plier
· Adjustable screw driver, plug spanner na
sanduku nzima ya spanner
· Kamba
· Fan belt
· Petrol au diesel na kitu kingine chochote
utakachokiona muhimu katika gari lako kwa safari
Kuvumbua kasoro
1. Kifaa au chombo kitakachokujulisha kuwa gari
lako lina kasoro ni Dash board.
2. Pia kwenye mwili wako viungo vitakavyokufanya
uvumbue kasoro ni
o Macho yako kwa kuona
o Sikio lako kwa kusikia
o Pua yako kwa kunusa
Unapogundua chochote cha tofauti kwa kutumia vitu hivyo juu
simamisha gari lako kagua na kugundua hitilafu.
Kuna aina tano “5” za Taa;-
· Full Light Taa kubwa – Taa hizi zina mwanga mkali na hutumika wakati
wa usiku ili kuona masafa marefu, endapo mbele hakuna kitu chochote
chenye mwanga mfano gari linguine ua pikipiki au baiskeli n.k
· Deem Light taa ndogo – Taa hizi hutumika kama mbele yako
kuna gari lililo kutangulia , pia kama mbele yako kuna gari lingine linakuja
unapaswa kutumia deem light au kama mbele yako kuna kitu chenye
mwanga mfano pikipiki au baiskeli au hata gari linguine
Hakikisha kuwa mwendo wa gari hauzidi mwendo wa mwanga wa gari
kwa msingi huo nenda mwendo sawa na wa taa zako
· Indicator ziko mbili kwa kawaida
Indicator ya kulia ni kwaajili ya kuonyesha kuwa gari linapinda
kulia au kwaajili ya kuomba nafasi ya Njia wakati unapotaka kulipita gari
linguine Overtake au kumzuia dereva wa nyuma asi Overtake
Indicator ya kushoto ni kwaajili ya kuonyesha kuwa gari
linapinda kushoto, kuruhusu gari la nyuma liweze kupita Overtake na kuonyesha
kuwa gari linataka kusimama au kupaki kushoto
· Parking light – Hutumika wakati gari linapokuwa limepaki
hususani wakati wa usiku, au wakati wa ukungu ukungu mvua ua vumbi, pia mara
giza linapoingia unashauriwa kuwasha Parking light ni hatari kama
unapark gari usiku bila kuwasha parking light kwani dereva wa gari nyingine
anaweza asikuone na akakugonga
· Brake Light – Hutumika kumjulisha dereva wa gari
la nyuma kwamba unapunguza mwendo au unasimama
UBADILISHAJI WA TAIRI
Utangulizi
Katika utaratibu wa kawaida ubadilishaji wa tairi unaweza
kufanyika katika njia kama mbili zifuatazo;-
· Kuisha kwa tairi – yaani baada ya tairi kulika
limeisha linahitaji kubadilishwa
· Pancha – wakati tairi linapopata pancha (Punctuare)
Kulika au kwisha kwa tairi
Kwisha au kulika kwa tairi ni jambo la
kawaida kutokana na msuguano wa tairi na ardhi, hivyo ni
vyema tairi linapokuwa limekwisha au liko kipara zibadilishwe na
kuvalishwa ganda ama mpira mwingine mpya ili kwamba ;-
a. Kuepuka usumbufu wa askari wa barabarani
b. Kulinda maisha yako nay a watu
wengine
c. Kuweka usalama wa gari
d. Kuwa na uhakika uwapo safarini na wakati wote
unaposhughulika na gari
e. Kupita sehemu yoyote bila ya kuwa
na wasiwasi
Kwa msingi huo basi ni muhimu kwa tairi za gari kuwa nzima
wakati wote ili kupunguza matatizo yaliyotajwa hapo juu.
Pancha (puncture)
Pancha hutokea wakati wowote na kwa tairi yoyote hususani zile
zilizolika kashata zake. Unapokuwa na pancha ni vyema kuzingatia yafuatayo,
iwapo utakuwa umekumbwa na pancha ni vyema kuzingatia yafuatayo iwapo pancha
imekupata kwenywe njia inayopitisha magari wakato wote zingatia maswala muhimu
yafuatayo;-
· Egesha gari pembeni mwa barabara
· Weka kibao au alama ya onyo kama unacho mbele
na nyuma ya gari kiasi cha mita 100 ili kuashiria tahadhari ya matengenezo au
uharibifuau marekebisho/Matatizo ya gari
· Weka vigingi au mawe kwenye tairi la
mbele na nyuma isipokuwa tairi lililopatwa na pancha
· Chukua wheel sperner na legeza nut za tairi
iliyopata pancha
· Chukua jeki tafuta sehemu itakayostahimili
uzito wa gari kama vile kwenye chassis Frame nyuma ya aksel au kwenye kiti cha
spring piga jeki juu ili tairi iachane na ardhi
· Chukua tena wheel spanner na malizia kufungua
nut za tairi ya pancha kisha ondoa tairi hiyo.
· Chukua tairi ya tahadhari (Spare tyre) funga
sehemu ya tairi iliyopata pancha, Funga nut kwanza kwa mkono kisha nut mbili
zinazoelekeana zikaze kwa kutumia wheel spanner, rudia tena nut zote kwa wheel
spanner, rudia tena nut zote kwa kwa wheel spanner kwaajili ya kuzikaza
usitumie bomba kwani unaweza kulegeza au kukata stud.
· Weka tairi lililopata pancha kwenye gari ondoa
mawe au vizuizi kwenye tairi, Ondoa vigingi ulivyoweka kwa
kuashiria magari mengine kuwa kuna matengenezo au matatizo
barabarani
· Washa gari kasha endelea na safari yako.
Ni muhimu kuhakikisha kwamba unapopata matatizo ya pancha pitia
kwa waziba pancha na kuziba tairi lako, iwapo tairi uliyoifunga ina kipara
rudishia tairi lenye kashata uliyoiziba pancha na tairi zako zinapokuwa
zimeisha kumbuka kufunga mipira mingine mipya
Vilevile kumbuka kutumia viegemezi supports kusaidiana na jeki
wakati wa kubadilishja tairi, ili kwamba iwapo jeki itashindwa viegemezi
vikusaidie kushika gari kuegemea chini upande wa tairi iliyopata pancha au
upande unaobadilishwa tairi
VITU MUHIMU KUELEWA NDANI YA GARI KWA DEREVA MWANAFUNZI.
1. Rejeta (radiator) – Kazi ya chombo hiki ni
kuhifadhi maji ya kupooza Injini
2. Oil – Kazi ya oil ni kulainisha vyuma
vinavyokutana kwenye gari, Oili ni muhimu sana kwenye injini. Kwani ukosefu wa
oil unaweza kusababisha injini kufa au kusimama (Knock)
3. Mafuta ya brake (Brake Fluid).- Kazi yamafuta
ya brake ni kusaidia gari liwe na brake pamoja na clutch. Kwa hivyo
unatakiwa kuangalia mafuta ya brake wakati wote pamoja na Clutch, unatakiwa
kuangalia mafuta ya brake wakati wote yawepo kwenye kihifadhio chake.
4. Betrii (Batery)- Kazi ya betrii ni kuhifadhi
moto na kutoa moto kwa kusaidia shughuli kama kuwasha taa, kuanza mwendo wa
gari (Starting) kuwa kwenye Moto/mwendo na kadhalika
5. Ignition coil;- Kazi ya ignition coil ni
kukuza moto utokao kwenye betrii na kuingia kwenye distributor nayo
inatoa huo umeme kwenye plugs ukiwa umepoa, plugs ndizo zinatoa moto kwenye
injini.
6. Distributor – Kazi ya distributor ni kugawanya
moto kwenye injini na kufanya gari liwe na mlio mzuri na nguvu, chombo hiki
kina waya tano na ukichomoa waya mmoja tu gari linbakuwa lina miss.
7. Plugs;- Kazi ya plug ni kuchoma Petrol kwenye
injini, Pulug inaposhindwa kuchoma inabidi uibadilishe ili kuepuka gari kuwa na
miss.
8. Fuel Pump – Kazi ya fuel Pump ni kuvuta mafuta
kutoka kwenye tank na kyapeleka kwenye Carburator
9. Carburator – Kazi yake ni kupokea
mafuta kutoka kwenye fuel Pump na kuyachanganya na hewa
kwa kipimo maalumu kilichowekwa na kwenda kwenye injini
10. Alternator – Kazi ya chombo hiki ni kuchaji betrii na kusaidiana
na betrii ili kutoa moto wa betrii na kusababisha betrii isipungue moto wakati
wote gari linapokuwa linatembea.
11. Self start. – Kazi ya self start ni kuwasha gari wakati gari
likiwa bovu na haliwezi kuwaka lenyewe, chombo hiki hifanya kazi wakati gari
linasukumwa na kushituliwa.
12. Gear box – kazi ya chombo hiki ni kubadilisha gea na kufanya
gari liwe na mwendo wa kasi zaidi au kupunguza kasi
13. Differential – kazi ya chombo hiki ni kugawa mwendo unaotoka
kwenye injini na kuupeleka kwenye matairi
14. Cut Out – Kazi ya cut Out ni kufanya Marekebisho ya umeme kutoka
kwenye Altarnator na kwa kipimo cha volt 12 kiingiacho kwenye betri.
SIFA ZA DEREVA.
· Ni lazima ajue Sheria za barabarani na kanuni
zake na kuzifuata
· Anatakiwa asiwe mlevi wa Pombe au vilevi vya aina
nyingine
· Anatakiwa kuwa mtu wa kulikagua gari lake mara
kwa mara
· Awe mtu wa kuwajali
watumiaji wengine wa barabara
· Asiendeshe kwa mwendo kasi wa kupita kawaida
· Ni lazima uwe mtu wa kujihami
· Ni muhimu unaposikia usingizi au kuchoka
usiendeshe gari
· Asiwe mtu wa mazungumzo yaliyokithiri kwenye
gari au wakati wa kuendesha
· Awe mpole na mwenye huruma
· Asitumie viburudisho wakati anaendesha
· Unapopigiwa simu ya mkononi ni muhimu kupark
pembeni ndipo uipokee.
Ufahamu kuhusu injini.
Injini ni chombo au mashine ambayo hubadilisha nguvu ya joto (Heat
energy) na kuwa nguvu ya mwendo (Mechanical Energy) kwa ujumla injini ina
sehemu kuu tatu zifuatazo;-
· Cylinder Head; Ni sehemu ambayo huwa upande wa
juu wa injini
· Engine block; Ni sehemu ya katikati ya
injini ambayo sehemu kubwa ni chuma
· Coil Samp; Ni sehemu ambayo huwa inakaa
chini ya injini, hii ni sehemu ambayoOil ya injini inakaa.
Spring;
Kwa kawaida spring katika magari huwa ni za aina kuu mbili
· Spring Bar – Hizi ni spiring za kawaida ambazo
huwa ni vipande bapa vya chuma
· Coil spring – Hizi huwa zimepindana kwa kwenda
juu zimejikunjwa mfano wa dawa ya mbu ya kuchoma.
Grease;
Ni mafuta mazito ambayo kwa kawaida hutumika kupunguza kulika
kwa vyuma yaani kupunguza msuguano “Friction” kwa kawaida Grease hupakwa sehemu
yoyote ambapo chuma hukutana na chuma kingine
Unapotaka kuzima gari kumbuka;
· Unapokuwa kwenye gia tahadhari usiachie clutch
kwani kuna uwezekano likazima ghafla,kwa hiyo zima ukiwa umakanyaga clutch na
brake halafu badilisha gia nambari moja, vuta hand brake kisha achia Clutch,
halafu achia Brake na mwisho ondoa ufunguo.
· Au ukitaka kuachia clutch kwaajili ya kuzima
unachofanya ni kuweka gia huru free ndio uachie clutch, kanyaga tena clutch na
badili gia kuwa Nombari moja, vuta hand brake na endelea kama hapo juu.
Pichani baadhi ya
vifaa vya gari kama vinavyoonekana Picha kwa hisani ya Rev. Kamote home Bible
Library. October 24, 2010.
UFAHAMU KUHUSU BIMA ZA MAGARI NA TARATIBU ZAKE.
Kwa kawaida sheria inaagiza kuwa magari yote ni lazima yawe
yamekatiwa Bima na kinyume cha hayo utakuwa umevunja sheria ya jamuhuri ya
muungano wa Tanzania. Lakini ni muhimu kufahamu kuhusu bima
Zipo aina kuu mbili za Bima
1. Third Party
Bima hii ni bima ambayo haitoi malipo gari linapokuwa limepata
ajali , Bima hii hueleweka kama bima ndogo, iwapo utapata ajali kati ya gari
mbili atakayelipwa ni mwenzako kama iwapo yeye anayo bima inayofanana na yako,
iwapo atakuwa na bima ambayo ni kubwa utalipwa kutokana na bima yake.
2. Comprihensive
Bima hii ni bima kubwa ambayo inakuwezesha kulipwa iwapo gari
yako itapata ajali iwayoyote na kwa kawaida utaratibu ufuatao huwa unafuatwa.
a. Dereva awe na umri unaostahili kuwa dereva au
kufanya kazi hiyo ya udereva
b. Leseni aliyokuwa nayo dereva kabla ya kupata
ajali ni daraja linalostahili kuendesha gari hilo
c. Leseni ya Derevahuyo lazima iwe
halali na ameipata kwa kufuata utaratibu wa kisheria, kinyume cha hayo Bima
haiatalipwa wala haita husika na hasara itokanayo na ajali hiyo
kabla ya kupata ajali ni daraja
Iwapo katika gari yako kuna redio ni muhimu kuikatia Bima yap
eke yake ili uweze kulipwa iwapo ajali itaharibu Redio hiyo.
UTARATIBU WA KUWASHA NA KUENDESHA GARI.
Unapomaliza kucheki gari yako unaingia ndani ya gari na kuiweka
free gari au gea , halafu unaweka switch on na kuangalia taa ya heater,
ikilazimika unawasha gari na baada ya hapo unaweka gea nambari
moja kasha unaachia clutch kidogo kidogo na utaona gari linaondoka
utaangalia gari mpaka lizungushe tairi raundi moja au zaidi halafu
utaachia clutch kabisa.
Gari linapokuwa barabarani unatakiwa uwe macho na kusoma alama
za barabarani na uwe mwangalifu usitoe macho tu unatakiwa kuwa makini kwa kila
alama za barabarani.
Unapofika njia panda au keepleft
Hakikisha kwanza
unasimama unaagalia kulia kwako kama kuna mwenye gari anakuja na
ameshafika unampisha apite na ambaye alikwisha kuingia
kwenye mzunguko, halafu unawasha indicator na kuonyesha mwelekeo wa kule
unakokwenda, utawasha ya kushoto kama unaingia njia ya kwanza.
Njia panda au keep left.
Kanuni za njia panda ua keep left.
· Unapaswa kusimama na kuangalia kulia kwako
kama gari imeshafika unaipisha ipite hususani ile ambayo imeshaingia kwenye
mzunguko
· Hakikisha kuwa unapiga indicator ya
kulia endapo hutaingia njia ya kwanza utabadilisha indicator ya
kuonyesha mwelekeo wa kuelekea unakokwenda
·
50
|
50
|
50
|
50
|
Unawasha indicator ya
kushoto kama utaingia kwa njia ya kwanza
- Kibao cha namba moja kimekataza usiende spidi zaidi ya spidi
hamsini
- Kibao cha namba mbili kimeruhusu kwamba unaweza kwenda zaidi
ya spidi hamsini
- Kibao cha namba tatu kimekataza kwenda zaidi ya spidi hamsini
- Kibao cha namba nne kimeruhusu kwenda zaidi ya spidi hamsini.
Kanuni ya njia mbili Double Road kama hakuna
keepleft unapaswa kubana upande wako kama umeshafika
sehemu ya upande wako wa kuchepukia wa kule unakokwenda
Kama kuna keep left utapaswa kwenda kama keep
lefti za kawaida .
Kama kuna barabara kuu
na njia panda unabana upande wako wa kushoto ambao ndio sauti yako halafu
unaelekea utakako.
1. Barabara hii uendeshaji wake ni sawasawa na
uendeshaji wa barabara za kawaida za double road , kwenye uendeshaji unapofika
kwenye kuchepuka unabana upande wako ambao utaingia
2. Barabara nyngine hazina barabara
kuu wala ndogo ,ukubwa wa barabara unategemea taa ya
kuongoza magari inapowaka
3. Kisha barabara hii ina ukubwa sana kuliko ile
ya double road ya kawaida.
4. Iwapo barabara hii inauwezo wa ku-ovaertake
pande zote ukiona hakuna hatari.
5. Halafu bara bara hii inayoongozwa na taa
inasema hivi;-
a. Taa nyekundu inazuia magari yasipite
b. Taa ya njano inasema ujiandae na kuondoka
c. Taa ya kijani inaruhusu kuondoka
d. Taa yam shale wa kijani inanukuu kuondoka
kwenda mshale unakoelekeza hata kama taa nyingine zinawak
Rangi nyekundu maana yake simama subiri nyuma ya mstari
buliochorwa hapa chini ya bara bara
Nyekundu na njano pamoja maana yake ni kusimama usipite mpaka rangi
ya kijani imetokea
Rangi ya kijani maana yake unaweza kupita lakini njia ikiwa ni
salama na pia ni muhimu kufanya tahadhari kwa watembea kwa miguu hususani
unapokuwa unageukia kulia au kushoto
Mshale wa kijani maana yake unaweza kwenda upande ulioelekezwa
na mshale huo na unaweza kufanya hivyo haizuru hizo taa nyingine
zinaonyesha nini
Rangi ya manjano maana yake simama nyuma ya mstari ulioko hapo
chini, unaweza kwenda ikiwa labda imekutokea iwapo ulikwisha kupita
huo mstari uliopo hapo chini hivyo au labda ulikuwa karibu sana.
MASWALI YA KUJIULIZA KWA DEREVA (MASWALI YA MDOKO).
1. Wakati unaendesha gari ikatokea imewaka moto
utafanyaje?
2. Unapopata ajali utafanyaje?
3. Ni vitu gani vya kuangalia kabla ya kuendesha
gari?
4. Eleza namna ya kugeuza gari katika barabara
kuu
5. Ni wakati gani unaporuhusiwa kuipita gari
iliyoko mbele zako?
6. Elezea umuhimu wa kukagua gari yako kabla ya
kuondoka
7. Kuna hajka gani wakati wa kupinda kona
kubadilisha gea?
8. Ni vitu gani vinavyotumia barabara
9. Ishara za barabara zina faida gani?
10. Taja sehemu nne ambazo ni makosa kuegesha gari
11. Taja sehemu tatu ambazo ni marufuku kupiga honi
12. Unatakiwa kusimama umbali gani nyuma ya gari lililosimama?
13. Unatakiwa kuwa umbali kiasi gani toka gari linalokwenda mbele
yako?
14. Utamjulisha vipi Dereva wa gari lilioko mbele yako kuwa unataka
kulipita wakati wa usiku?
15. Taja mambo manne unayotakiwa kujihadharisha unapoendesha gari
16. Utajuaje kama unaingia mjini au unatoka mjini kwenda nje ya mji?
17. Ni mwendo kiasi gani unatakiwa kuendeesha unapokuwa nje ya mji?
18. Taja sifa anazotakiwa kuwa nazo Dereva?
19. Unatakiwa ufdanye nini kabla ya kupinda kulia?
20. Ni gari la upande gani lenye haki ya kupita kwenye kona au
mzunguko?
21. Utafanaya nini kama unataka kupinda kulia iwapo kuna gari
linalokuja mbele yako ?
22. Taja vyeti unavyotakiwa kuwa navyo unapoendesha gari
23. Ni mambo gani yanaweza kusababisha ajali taja matatu
24. Utafanya nini Kama gari litazima ukiwa mlimani?
25. Utaangalia nini kabla ya kuondoa gari lako?
26. Alama ya mstari mweupe ulionyooka barabarani inakuonyesha nini?
27. Alama ya mstari mweupe ulioachana achana unakuonyesha nini?
28. Utafanya nini kablaya kufika mahali unapotaka kupinda?
29. Utafanya nini unapopita mahali penye shule pasipo na alama ya
kivuko cha watoto wa shule?
30. Ni wakati gani unapotumia kioo cha kuangaliua nyuma unapoendesha
gari?.
31. Unapaswa kufanya nini unapoendesha gari wakati wa usiku?
32. Elezea jinsi taa za magari zinavyofanya kazi?
33. Utafanya nini iwapo gari lako limeharibika barabarani?
34. Ni ishara gani utaiona kama mtu mashuhuri anapita na utafanya
nini?
35. Mahali gani unapaswa kuwapisha waendao kwa miguu?
36. Utafanya nini kama unasikia usingizi unapoendesha gari?
37. Ni sehemu gari za viungo zinatakiwa kuwa katika hali nzuri kabla
ya kupata lesseni?
MASWALI KWA MADEREVA WA MAGARI YA ABIRIA:
1. Ukiwa dereva unatakiwa uwe na tabia gani kwa
abiria?
2. Je dereva wa abiria anatakiwa kuvuta sigara
katika gari anapoendesha kwa nini?
3. Unapaswa ufanye nini ukiwa dereva wa gari la
abiria wasafiri wanapopanda ndani ya gari?
4. Utampa taarifa gani askari iwapo
atakusimamamisha na kukuhoji?
5. Kama gari yako inashukiwa kuwa ni mbovu na
kukamatwa na askari utafanya nini?
6. Je ukiwa ni dereva wa gari la
abiria unaruhusiwa kuzungungumza na mtu yoyote kwa nini?
7. Utaegesha vipi gari kama abiria wanataka
kuteremka?
8. Kabla hujaendesha gari la abiria unatakiwa
ufanye nini?
9. Utahakikishaje kuwa abiria wote wamekaa sehemu
zao kabla ya kuondoka ?
10. Ni vitu gani visivyoruhusiwa kupakiwa katika gari la abiria?
11. Vitu gani vinatakiwa kuwemo katika gari kwa tahadhari ya ajali
au moto?
12. Unatakiwa kwenda mwendo gani mjini na mwendo gani nje ya mji/
13. Kila abiria anaruhusiwa kuchukua mzigo au uzito gani
14. Kuna hatari gani iwapo gari litazidisha mzigo?
15. Ipo haja ya kukimbizana ili uwahi abiria? Hatari zake ni zipi?
16. Je abiria ana haki ya kutoa ushauri anapoona mambo yananyofanywa
si sawa?
MASWALI KWA MADEREVA WA MAGARI YA MIZIGO.
1. Gari linalobeba mizigo au mafuta lazima liwe na
vifaa gani?
2. Gari linalobeba vifaa vya hatari kama baruti,
sumu na gas linatakiwa kuwasha taa ndogo?
3. Je ni wakati gani unapotakiwa/Kuruhusiwa
kuendesha gari lenye vifaa vya hatari?
4. Kabla ya kuendesha gari lenye vitu vya hatari
unapaswa kuangalia nini?
5. Iwapo gari lako limeharibika katikati ya
barabara unapaswa ufanye nini?
6. Sheria inasema nini juu ya utumiaji wa taa
ndogo au ni wakati gani unatakiwa kuwasha taa ndogo
7. Abiria wanagapi wanaoruhusiwa kupakia katika
gari la mizigo?
8. Ni barabara gani utakalopitisha gari la mizigo
mjini
9. Ni sehemu gani za muhimu za gari zinazotakiwa
kuwa madhubuti kwa kubeba mizigo?
10. Eleza jinsi unavyotumia taa za gari lako usiku kama kuna gari
nyingine inakuja mbele yako?
11. Ishara gani utaitumia unapolipita au kupishana na gari lingine?
12. Utafanya nini iwapo utakutana na gari lingine karibu ya daraja?
13. Utatoaje ishara ya kusimama?
TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA BARABARA;
1. Endesha kistaarabu.
Ada ya mja kunena , Muungwana ni kitendo, Basi kama ni hivyo
onyesha uungwana wako kwa kuendesha kistaarabu barabaraniUwe mpole na
uwafikirie watumia barabara wenzako, uwe mvumilivu, mtulivu, usiwe na papara
lazima uwajali watu na madereva wengine unapoendesha barabarani.
2. Fikiri kabla ya kuteenda.
Fikiri sana kabla ya kuamua, uwe na uhakika na kila hatua ya
utekelezaji , usije ukadhani kuwa ni kosa lako tu linaloweza kuleta hatari
barabarani, Hapana uwe tayari pia kuayamaliza na kuyaepuka makosa ya watumiaji
wengine wa barabara
3. Mkono dirishani.
Unapoendesha au kuendeshwa usitoe mkono dirishani na kuuacha
hapo hapo katika hali ya kupumzika huku kisukusuku au kiwiko cha
mkono kikiwa kimejitokeza nje ya dirisha
4. Watoto ,Vilema na wasiojiweza.
Ni muhimu kuchukua tahadhari zaidi dhidi ya watoto wadogo ,
vilema na ndugu wasiojiweza, hususani unapokuwa barabarani, hao wanahitaji
huruma zako, moyo , msaada na uelewa wako wa dhati.
5. Ishara alama na michoro ya barabarani.
Zijue ishara zinazotumika barabarani, jifunza zielewe ,uzimudu
na kuziheshimu alama na michoro yote ya barabarani.
6. Michezo Barabarani.
Wafundishe watoto namna ya kuziheshimu barabara na hasa namna ya
kuzivuka kwa usalama , uiswaruhusu watoto kucheza barabarani au
karibu na barabara, Aidha usiwaruhusu watoto wadogo kuvuka barabara wakiwa peke
yao bila kuongozwa.
7. Dereva akiwa kazini;
Lazima abiria ajizuie kumyumbisha dereva mawazo
yake akiwa kazini,usibishane naye wala kupiga gumzo naye
wala kuimba kupiga kelele au kumshitusha na au kufanya kitendo chochote kile
kitakachoathiri mawazo yake anapoedesha.
8. Takataka.
Usitupe vipande vya sigara au takataka zozote barabarani
WAENDAJI BARABARANI.
a). Kutembea.
1. Kutembea barabarani;
Kila mara tembea kwenye kijinjia cha waendaji kwa
miguu kama kipo, kama hakipo tembea nje ya barabara ili au ukingoni
mwake upande wa kulia mwa barabara ili uyaone kwa
urahisi magari yanayokuja mbele yako, ukifanya hivyo utapata nafasi
kubwa ya kuyakwepa magari yanayojongea uliko.
2. Kutembea na
mtoto;
Usimwachie mtoto aende kwa imani yake mwenyewe, mshike kwa mkono
wako wa kulia na utembee kati yake na barabara upande wa magari.
3. Maandamano
ya watu;
Kundi la watu linapofanya maandamano barabarani lipite upande wa
kushoto wa barabara , wawepo watu wa kutahadharisha
usalama na kuwatahadharisha watumia bvarabara wengine .
4.Kuzuia njia ;
Usiwazuie wenzako kwa kusimama katikati ya njia ya waendao kwa
miguu kwa sababu yoyote ile.
5. Kuzurula barabarani;
Usisimame, kuzubaa kuzurula au
kutangatanga barabarani hasa kwenye kona na sehemu
yoyote pofu au sehemu nyingine yeyote ya barabara ambapo dereva
hawezi kukuona kwa urahisi.
6. Kuelekea barabarani;
Uwe mwangalifu sana utapoelekea kwenye Barabara, angalia kwa
makini kuhakikisha kuwa hakuna gari linalojongea upande uliko kaa chonjo.
Kuvuka Barabara;
1. Kuvuka barabara ;
Kabla ya kuvuka barabara simama
kwenye ukingo wa barabara kwanza halafu angalia kulia ,
kushoto , halafu kulia tena kama hakuna gari vuka moja kwa moja
mpaka ukingo wa pili usivuke kimshazari.
2. Barabara kwenya gema au kisiwa;
Kama barabara ina gema katikati simama hapo kwanza baada ya
kuvuka nusu ya kwanza ya barabara, hakikisha kuwa madereva wa upande wa pili wa
barabara wamekuona hasa kama kuna giza.
3. Kuvuka kwa kukurupuka ;
Usivuke barabara kama mwizi au mwenda wazimu na hasa usivuke
mahali pengine popote kama kivuko cha waendao kwa miguu kipo karibu.
4. Kuvuka kwenye kiyuo cha magari;
Usivuke barabara kwenye kituo cha kupandia au kuteremshia
abiaria na hasa mbele au nyuma ya gari, abiria anapoingia au kutoka kwenye
gari.
Kivuko cha pundamilia
1. Kivuko cha punda milia
Hiki ni kivuko cha waendao kwa miguu. Usivuke kituo hicho mpaka
umehakikisha kuwa abiria wamekuona na wapo tayari kukupisha ,
unapovuka pepesa macho kulia kushoto na kulia tena , kama tahadhari
kwa madereva ambao inawezekana wameshindwa kusimama, chukua
tahadhari wakati wote.
2. Kivuko chenyae kisiwa
Kuna vivuko vingine vya watembeaji kwa miguu vyenye visiwa
katikati ya barabara , endapo kisiwa kipo katikati ya kivuko cha punda milia ,
vuka kila nusu ya kivuko hicho kama kivuko kamili kinachojitegemea.
Vivuko Vinavyoongozwa.
1. Vuvuko vinavyoongozwa na taa.
Unapovuka mahali panapoongozwa na taa fanya hivyo tu taa ya
kuvuka ikiwaka
2. Kivuko kinachoongozwa na askari.
Endapo Askari wa kuongoza magari haya yupo ni muhimu kuvuka
barabara tu askari akikutolea ishara .
Kupanda na kuteremka.
1. Kupanda na kuteremka kwenye gari;
Usidandie gari wala kuning’inia. Aidha usipande wala kushuka
kwenye gari likiwa bado kwenye Msururu wa magari ngojea hadi litakaposimama na
kuegeshwa pazuri au kwenye kituo kilichoidhinishwa.
2. Kuingia na kutoka kwenye gari.
Hakikisha kuwa unaingia na kutokea upande wa kushoto
wa gari,ikiwa mlango wa kutokea uko kulia , basi hakikisha usalama
wako kwa kuangalia kulia na kushoto na ukitoka usivuke barabara mara
moja.
Usiku, vizuizi na Mkokoteni.
1. Matembezi ya usiku.
Unapotembea usiku;
Unapotembea usiku au kwenye giza , haklikisha kuwa umevaa nguo
nyeupe au zinazoonekana kwa urahisi gizani au shika kitu
kinachong’aa, hali hii ni muhimu zaidi kwa barabara za vijijini.
2. Kuvuka vihunzi.
Usivuke vihunzi au vizuizi vyovyote vilivyojengeka , Pembeni mwa
barabara ,unapotaka kuvuka.
3. Mikokoteni.
Wenye mikokoteni pia hawana budi kuziheshimu sheria na kanuni
zote za barabarani, sukuma mkokoteni pembeni kabisa mwa upande wa kushoto wa
Barabara , toa ishara shii au kuvuka kwenye njia panda,
KWA MADEREVA WOTE;
Afya , usalama wako na wa gari;
1. Afya ya dereva.
Usiendeshe gari isipokuwa kama una uhakika wa
afya yako ya mwili na akili yako , Ni lazima mwili wako na fikira
zako ziwe katika mtiririko mmoja ili kusababisha hali ya usalama barabarani,
ulevi wa pombe , madawa ya kulevya na uchovu huathiri uwezo wa
kufikiri kwa makini , kupanga , kuangalia na kuamua sawia.
2. Hali ya gari.
Hakikisha kuwa gari lako lipo katika hali nzuri kabla
ya kuliweka Barabarani, ukaguzi wa marakwa mara wa Breki, usukani, magurudumu
na indiketa ni wa lazima , Aidha hakikisha kuwa kioo cha
mbele ni kisafi na vipanguso na Wepa navyo vinafanya kazi
kila wakati.
3. Ubebaji Mizigo.
Usipakie au kubeba gari lako mizigo mingi na mizito kupita kiasi
kinachokubalika kwa wastani.
4. Shehena kubwa.
Ukipakia mzigo au shehena na ulio zagaa au kujipenyeza pembeni
au nyuma unatakiwa kuwa mwanagalifu sana kwa mwendo. Na
ni lazima pia kuweka alama za kuwaonya watumiaji wengine
wa barabara kwa kufunga kitambaa chekundu, kama ni mchana au taa nyekundu kama
ni usiku.
5. Kofia ya usalama.
Ni vizuri kuvaa kofia ya Usalama kwaajili
ya kujikinga kichwa dhidi ya ajali ya kugongwa kichwa , kila
unapoendesha chombo cha moto kama pikipiki n.k.
MADEREVA WAPYA NA MANJU;
Usikimbilie kuendesha gari subiri na kuhakikisha kuwa
unafundishwa na mkufunzi aliye taalamika na aliyelimbikiza ujuzi na
uzoefu wa kutosha. Usianze kwa papara utaishia pabaya. kumbuka daima kuwa
kuliendesha gari ni kitu rahisi sana na karibu kila mytu anaweza
kama akitaka na akaweza katika siku chache tu . Kinachofanya mafunzo
yawe ni kitu muhimu na cha lazima ni haja ya kujifunza
mbinu mbalimbali za kuthibiti barabara , mazingira na gari lenyewe,
ni vizuri kujifunza kuanzia hatuia za awali, Tabia
njema katika udereva ili hatimaye ujuzi na
uzoefu wako ujengwe juu ya msingi imara itakayokusaidia kuziepuka
ajali za barabarani kwa urahisi zaidi. Ili uweze kuwa
dereva bora mwenye msimamo wa
usalama barabarani, huna budi kuanza tangu
mapema kujifunza na kuyazingatia kati ya mambo
mengi muhimu yafuatayo;
1. Kuzijua kanuni
Ni lazima uujue Udereva katika mapana na marefu yake
uzijue uzikariri na kuzizingatia sheria na kanuni zote za usalama barabarani
kujua huko kuambatane na makusudi ya kuzitekeleza kanuni hizo ipasavyo.
2. Uwe dereva wa kujihami;
Ni vema ikumbukwe kuwa hata Dereva bora, anayejulikana kwa
ustadi wake anaweza akasababishwa na watumiaji barabara wengine na akapata
ajali.Falsafa ya dereva wa kujihami inaelekeza kuwa dereva asiridhike na kujua
kwake sheria na kuzitekeleza kanuni tu, wala asifikiri kuwa madereva na
watumiaji barabara wengine wote wanazijua na wataziheshimu sheria ipasavyo.Ni
lazima aendeshe huku akiwa tayari kufidia na kurekebisha makosa yaw engine kwa
sahihi za kuepusha shari na kuleta hali ya maelewano na usalama barabarani.
3. usalama barabarani;
Dereva wa kujihami, kamwe haendeshi kwa kuwakomoa wanaofanya
makosa barabarani.Udereva wa kujihami ni udereva wa kutumia akili.
4. heshima kwa wengine;
Ni wajibu kwa dereva kuonyesha uungwana na kumheshimu kila
mtumiaji barabara.Mwenye gari ndogo au kubwa,pikipiki, baisk eli ,
mkokoteni,n.k mpishe mwenye haraka au shida kila inapobidi, hata kama wewe
ndiye mwenye haki ya njia.
5. ajali za barabarani;
Jitahidi kufahamu kuwa, ajali za barabarani hazitokei tu, bali
husababishwa.Mara nyingi hutokea ikiwa ajizi imefanywa dhidi ya misingi hiyo,
jizoeze na jizatiti kuibaini ukiwa barabarani.
6. lijue gari lako;
Jitahidi na uwe na dhamira ya kuliijua gari lako
lilivyoundwa.Ijue mitambo iliyopo ndani ya gari, viungo vyake na sehemu
nyingine nyeti,zikiwa ni pamoja na maguridumu. Hali hii itakuweaesha kuwa na
staha ya aina Fulani kabla hujaamua kwenda kasi Fulani na kuzuia uwezekano wa
ajali hasa zile zenye asili ya kifundi.
UDEREVA WA KUJIHAMI;
Kila siku madereva wote hupambana na hatari ambazo haziwezi
zikamhakikishia dereva usalama wake na wa gari wakati wote.Hatari hizo
zinahusiana na hali ya gari, tabia na hulka ya waenda kwa miguu na hali ya
barabara yenyewe.Lakini tofauti ya elimu,tabia hulka na ujuzi wa madereva
wanapokuwa barabarani humpa mtihani mgumu sana Dereva bora na stadi.Azma ya
usalama barabarani,imejengwa juu ya mategemeo ya kuwa na dereva wa kujihami,
ambaye atahakikisha usalama barabarani,imefengwa juu ya mategemeo yakuwa na
dereva wa kujihami, ambaye atahakikisha usalama barabarani wakati wote.
Dereva wa kujihami (tazama maana yake hapo juu Ibara Na.2)
Ni mtaalam wa medani za barabarani na anazo mbinu kadhaa
anazozitumia katika kukwepa hatari na kujiokoa yeye gari lake na watumiaji
barabara. Kwa jumla dereva wa kujihami huzingatia mambo matatu kabla hali
haijamshinda, nayo ni;
a. Hutambua
hatari-uwezo wake wa kuhisi na kutambuahatari kubwa.Haendeshi kwa kudhani au k
Udhani au kubahatisha, bali kwa kuwa na uhakika. Zing’amue hatari mapema na
amua kuziepa hatari na na vikwazo vya barabarani.
b. Huelewa mbinu za uzuiaji-atajitahidi kuepuka
hatari ama kuzuia janga kutokea.Jifunze mbinu mbali mbali na uzitumie kwa
wakati ufaao au zinapohitajika.
c. Huchukuahatua –huendesha kwa kujikiri mbele
zaidi na akinusa tatizo huamua kutekeleza mara moja. Usingoje yatokee, epusha
shari, wala usidhani kuwa atasimama yeye.Simama wewe.
TAHADHARI KWA JUMLA;
Watoto wadogo na hata wale wanaokwenda shule wamo hatarini zaidi
kuliko watu wazima.
Walindeni na wafundisheni juu ya usalama barabarani.Wazee na
wakongwe nao ni wagumu kuwaza na kumaliza kasi ya mwendo wa vyombo
vya moto vinavyowajengea wafikirieni hao pia.
Kumbukeni hali ya afya zao, udhaifu wa macho yao, uzito wa
kutembea kwao.
Waendeshaji wa vyombo nao wajione kuwa wazima wa afya kabla ya
kuendesha.Aidha magari yanayoendeshwa barabarani yawe mazima, katika hali nzuri
na yakaguliwe mara kwa mara ili yasisababishe ajali za barabarani.Taa,breki
,usukani, magurudumu na viungo, vingine vithibitishwe kuwa vipo katika hali
nzuri.
LESENI;
Leseni ni hali ya kisheria inaokuruhusu mhusika kuthibiti au
kuendesha vyombo vya moto katika darafa lililoonyeshwa katika
leseni.Kwa hiyo pamoja na kuwa na leseni bado dereva anawajibika kujua mbinu
mbalimbali za uzuiaji na kujifunza, kuzikariri na kuzizingatia kanuni na sheria
mbalimbali za usalama barabarani.
Aidha ni vema ikumbukwe nia yautahini wa udereva ni kuhakikisha
kuwa, mtahiniwa anazifahamu sheria za udereva bora na kwemba amefundishwa vya
kutosha, amefanya mazoea ya sheria kiasi cha kuinukia kuwa dereva bora ambaye
siyo hatari kwakebinafsi na kwa watumiaje barabara wengine.
STAHILI YA LESENI.
Chini ya miaka 16-Hapati leseni kabisa.
Miaka 18 hadi 20-Leseni za pikipiki na magari madogo na gari za
biashara.Lakini siyo magari ya abiria wala yale makubwa ya mizigo.Miaka 21 na
zaidi –Leseni za pikipiki gari ndogo magari makubwa ya mizigo nay a abiria.
KUMBUKUMBU
Mwombaji wa leseni za kuendesha magari ya abiria au
magari makubwa ya abiria analazimika kwanza kupata cheti cha kuthibitisha uzima
wa macho yake kutoka kwa Daktari.
USALAMA WA GARI;
Usalama wa gari unahusu yafuatayo;
i. Kuibiwa
au kuharibiwa kwa gari.
ii. Kuibiwa kwa baadhi ya vifaa vilivyo sehemu ya
gari hilo
iii. Na wizi unaokuwa ndani ya gari hilo.
MAMBO YA KUZINGATIA;
1. Usiache swichi ndani ya gari lako na ufunge
usukani unapotoka nje au kuegesha.
2. Funga gari lako unapokuwa hulitumii k.m
ukiliegesha.
3. Funga vioo na milango kila unapoegesha au
kutoka. Usiache nafasi yoyote.
4. Ondoa vitu vyote vyenye thamani au vifungie
kwenye buti japo utakuwa umefunga milango na madirisha.
5. Vioo vyote viandikwe namba ya gari.
6. Hakikisha namba ya gari lako limewekewa bima.
7. Tunza vizuri hati ya gari yako.kama hati ya
kusajiliwa.Bima pamoja na anwani (jina)la udereva.Hivi vinaweza kumwezesha
mwizi kuuza gari lako kwa urahisi zaidi.
8. Watu wanaotiliwa mashaka kutokana na tabia zao
wasipewe leseni.
9. Tegeshea mtambo wa kuzuia wezi kama gari linao
kama huna unaweza kuuweka.
10. Weka kumbukumbu namba za vitu vya gari lako , kama radio na
kadhalika
11. Jihadhari na watu wanaoonekana kuwa na nia mbaya na gari lako ,
ikiwezekana jihami kwa kutoa taarifa polisi
12. Funga tenki la mafuta kwa kifuniko imara ili wezi wasiyaibe au
kuyaongeza mafuta katika gari lako linapokuwa limeibiwa au kuporwa.
13. Usiwaache watoto au watu wasiojiweza kwenye gari lililofungwa au
lisiloingiza hewa
14. Usiku egesha gari lako gereji au sehemu yenye mwanga wa kutosha
utakaokuwezesha kuwaona wezi kwa urahisi zaidi, lifunge vizuri.
15. Tafakari juu ya usalama wa gari lako na usalama wako mwenyewe
kabla hujatoka kwenye gari lako.
DARAJA ZA LESSEN.
Daraja la A; Pikipiki za aina zote
Daraja la B; Magari ya aina zote isipokuwa ya Biashara ya Mizigo
naya abiria
Daraja la C; Aina zote za magari Tazama kumbuka hapo juu na
mizigo
Daraja la D: Aina zote za magari sipokuwa magari ya mizigo na
Abiria
Daraja la E: Aina zote za magari isipokuwa ya abiria
Daraja la F: Magari ya shughuli za ujenzi
Daraja la G: Magari ya katika shughuli za migodi na mashamba
MATAYARISHO YA UTAHINI:
Baada ya kujifunza vema Udereva, kuzijua na kuzitafakari sheria,
ukiambatana na mazoezi mazito chini ya mkufunzi wa udereva, hatua ifuatayo ni
ile ya kwenda polisi kutahiniwa.
Uko kwenye kituo cha utahini mtahiniwa atawajibika
kumthibitishia mtahini kuwa anao uwezo wa kukiendesha chombo kwa
uhakika na bila kubabaisha , Aidha amthibitishie mtahini kuwa
anazijua sheria na kanuni zote za usalama barabarani.
Katika kuelekea huko kwenye kituo cha utahini mtahiniwa ajiandae
na maswala yafuatayo.
a. Lessen ya Muda (Provisional)
b. Gari sahii kwa adaraja la lessen unayoiombea
na gari liwe zima lenye bima na lessen hai ya
njia
c. Stakabadhi ya ada ya utahini kutoka katika
ofisi ya serikali ya mapato (Revenue). Na ada yoyote nyingine kama ipo
d. Chunga muda na kituo ulichopangiwa kwa utahini
kwani ukichelewa utahini utaahirishwa.
UTAHINI;
Kumbuka daima kuwa baadhi ya mambo ambayo mtahiniwa anatakiwa
kuyathibitisha katika majaribio au utahini ni kama yafuatayo;-
i. Umahiri wa kuliongoza gari katika barabara
ya kawaida na katika misururu ya magari mengine
ii. Umahiri wa kuyapita magari mengine, utumiaji
wa aina mbalimbali za barabara na namna ya kutawala kasi ya mwendo.
iii. Umahiri wa kona na uendeshaji wa kurudi kinyumenyume.
iv. Uendeshaji wa magari ya aina
mbalimbali
v. Alama ya michoro ya barabarani pamoja na
sheria na kanuni za usalama Barabarani
Onyo kwa wanaotaka kujifunza udereva.
1. Hakikisha kuwa unafundishwa na mkufunzi
aliyetaalamika vya kutosha katika fani ya udereva.
2. Usikubali kufundishwa na dereva anayeendesha
kwa kubahatisha na mwenye kuleta mbwembwe njiani au asiyestaarabika.
3. Usikubali kufundishwa kwenye mkweche wa gari
yaani gari lisilokuwa katika hali nzuri.
Kumbuka kuendesha gari si kitendo rahisi sana ,Lakini suala siyo
mradi kuendesha bali muhimu ni kujifunza mbinu mbalimbali zitakazokuepusha
na uwezekanao wa majanga uwapo barabarani.
UDEREVA BORA;
Dereva bora yeyote Yule lazima awe amepitia mafunzo ya udereva
kikamilifu kutoka kwa mkufunzi aliyetaalamika vilivyo na mwenye ujuzi wa
kutosha.
a. Dereva bora ni lazima kwanza ajihusishe
na gari lake ipasavyo, katika azima hiyo ni lazima azingatie
yafuatayo;-
1. Kagua gari lako na hasa chunguza magurudumu,
honi, milango, maji,mafuta ,taa zote pamoja na za
ishara hii iwe tabia yako.
2. Rekebisha chochote kibovu kabla ya kuendesha
kwa mfano kiti cha kukalia, vioo, milango n.k.
3. Jaribu breki zako kama zinafaa na uwe na tabia
ya kufanya hivyo kabla ya kuendesha wakati wote.
4. Uondokapo uhakikishe kuwa hakuna vizuizi mbele
, nyuma na hata chini ya mvungu wa gari.
5. Uendeshe tu ukiwa na uhakika na iwapo mgonjwa
jizuie sana kuendesha gari.
b. Kadhalika dereva bora hana
budi kuzingatia kanuni zifuatazo kwa usalama wake na
watumiaji wengine wa barabara , baadhi yake ni;-
1. Tuliza akili na fikira zako.
2. Jifunze zikariri na uziheshimu sheria na
kanuni za usalama barabarani.
3. Mwili na fikira zako barabarani ziwe kitu
kimoja
4. Fikiria kwanza kabla ya kutenda
5. Jizoeze kujizuia na uwe mwanagalifu
sana barabarani
6. Uwe mwanagalifu na mwepesi kabla ya kufanya
uamuzi
7. Uwe na ujuzi na uzoefu wa kutosha wa gari lako
8. Uangalifu zaidi unahitajika unapoendesha gari
mpya au ambayo sio yako.
9. Endesha kwa akili, nenda kwa kasi mahali
panapohitajika na panapo faa kwa wakati unaofaa tu
kumbuka kuwa mjinga yeyote anaweza akaenda kasi na akapata
ajali.
10. Tumia honi kwa akili na toa ishara zinazoeleweka tu.
11. Uwe mwenye heshima na adabu kwa watumiaji wa barabara wote.
12. Usiendeshe gari bovu aslani.
c. Endesha kwa staha ;
1. Kumbuka daima kuwa mjinga yeyote anaweza
kuiwasha gari , akaiendesha akaigeuza lakini kwa dereva bora
huwajibika kwa hayo tu.
2. Endesha kwa juhudi, maarifa na uangalifu ili
kuepusha ajali, unapoelekea kwenye njia panda , kipingamizi chochote
au mzunguko keep left au kupita kwenye maeneo ya shule, hospitali na mahali
popote hatari na ni muhimu kukumbuka yafuatayo;-
I. Nenda kwa kasi ya kawaida itakayokuwezesha
kusimama ikitokea hatari.
II. Toa ishara (Indicator) mapoema ili wenzako
wajue makusudio yako.
III. Jua namna ya kuzitumia barabara za aina
mbalimbali kwa usalama na bila kujihatarisha mwenyewe au kuhatarisha wengine.
Kadhalika unaweza kuepukana na ajali za barabarani ukizingatia
vipengele vifuatavyo;-
a. Zijue hatari zinazokukabili barabarani,
unapoelekea au ukifika kwenye hatari angalia kioo chako kwanza.
b. Utoe ishara sahii kuwajulisha wengine
unachotegemea kufanya.
c. Punguza mwendo kabla hujapiga breki , na
tazama kioo tena.
d. Panga gia sahii, pita kwa uangalifu.
e. Rekebisha kasi ya mwendo wako kwa kuchunguza
kasi ya mwendo wa magarai mengine
f. Kama kuna watumiaji wengine wa barabara
wengine barabarani basi waonye kwa ustadi.
g. Ukiisha kuipita hatari yoyote ile ondoka upesi
hapo kwenye sehemu hatari.
Kwa maelezo zaidi ya upitaji salama kwenye sehemu za
hatari kama kwenye njia panda soma
amelekezo kwenye kitabu cha medani za barabarani cha H.B.
Bantu ukurasa wa 37 hadi 42.
Dereva anbapaswa kuliweka gari kwenye msimamo au mkao
mzuri wa barabarani anapoendesha gari lake kwa
kasi ya mwendo wa staha na akione kipingamizi chochote
barabarani kama watu , mawe, n.k, apunguze mwendo na kuwa tayari
kusimama
Ukiwa unaendesha swala la uangalifu ni muhimu sana siku zote
.Tumia macho yako wakati wote, Usilipite gari linguine (Overtake) sehemu
a. Yenye kona
b. Yenye mlima
c. Yenye kivuko cha punda milia au kwenye kivuko
cha Reli
d. Kwenye njia panda
e. Kwenye daraja
f. Kwenye barabara nyembamba.
Ukifanya ajizi utapata ajali na kuhatarisha maisha yako nay a
wengine aidha ni vema ukumbuke tena kuwa;-
a. Uwe makini barabarani usiondoe macho yako
barabarani
b. Kila mara pepesa macho kwenye kioo
c. Kila mara waone watumiaji wengine wa barabara
kama chanzo cha ajali hivyo chgunga mienendo yao.
d. Penye gari lililo simama mbele yako
chunguza kwa makini kama kuna anayevuka barabara
e. Chunga sana watoto na wazee, wanaweza kuvuka
barabara bila ya kuchukua tahadhari
f. Unapoyapita magari yaliyo
pembeni mwa barabara yapite kwa uangalifu sana
g. Usihisi tu kuwa dereva mwengine atakupa
hali ya njia au kukuruhusu upite Subiri mpaka afanye hivyo.
h. Usiendelee na mwendo kama huoni
mbele
i. Pita kushoto Keep left unapoendesha gari bana
upande wa kushoto wa barabara ispipokuwa unapolipita gari linguine.
j. Kulipita gari linguine Overtake kunaweza
kufanyika unapokuwa umahakikisha kuwa ni salama kufanya hivyo na kuwa upeo wako
wa mchoni mkubwa na hakuna msururu wa magari au magari yanayongojea.
k. Nenda polepole kama huoni
mbele sawasawa au huna uhakika na hali ya
barabara na unapopitwa na magari mengine punguza
mwendo na jitayarishe kusimama kila inapobidi.
l. Jihadhari na kutaka kuwahi kwani kunaweza
kusababisha kuyavuka magari mengine na utajilazimisha kukatisha barabara kwa
nia ya kuyawahi magari mengine jambo ambalo linaweza kukusababishia usiyawahi.
m. Kubadili njia kwenye barabara ya njia nyingine, usibadili kutoka
njia moja kwenda njia nyingine bila uangalifu , angalia kioo , toa
ishara chunguza kwa macho.
UNAPOENDESHA INAKUPASA.
Inakupasa uwe katika nafasi ambayo inakuwezesha kutumia na
kuongoza gari lako ambavyo unaweza kuona sawasawa , barabara mbele
na magari mengine n.k. Umpe heshima yule ambeye yuko katika
kivuko cha kuvukia barabra kwa miguu.
Angalia sheria za barabara na ishara (Traffic Signs) Simama
ukitakiwa na Ofisa wa Polisi kufanya hivyo, angalia ngalia kama taa
zako ndogo na za pembeni zinawaka wakati wa usiku, haikupasi kuendesha bila
tahadhari kwa mwendo ambao unaweza kuhatarisha watu, ukisimama
inakulazimu kuzima injini na breki kabla ya kuacha gari, zima taa
kunwa za mbele wakati wa usiku lakini hakikisha kuwa taa ndogo
zote za nyuma na mbele zinawaka , Ikitakiwa na Polisi onyesha lessen
yako ya kuendesha na cheti cha bima Insurance kwa ukaguzi.
Inawezekana kuvitoa popote kwenye kituo chochote cha pilisi
unachopendaHaikulazimishi kuendesha gari lako unapokaribia kivuko cha watembea
kwa miguu , kusimamisha moto wa gari linalokokotwa na gari linguine
penye “on waiting” yaani hakuna kungoja palipokatazwa kusimama au
kusimamisha magari, kupiga honi gari likisimama . aidha sheria inataka
upatikanapo na hatari yoyote ambayo ni hasara au jeraha kwa mtu yeyote au
gari nyingine au mnyama ni lazima kusimama na saidia kama
kuna mtu aliyeumia na eleza ripoti polisi bila subira, Kwa madereva wa pikipiki
skuta na waendeshaji wa baiskeli baada ya mengi yanayotakiwa katika
sheria zinazohusu madereva wa magari pamoja na zile
zinazohusu vivuko vya waenda kwa miguu pia zuinakuhusu , haikulazimu
kuchukua watu zaidi ya mmoja kwa mshine ya miguu miwili na abiria
kuketi kwa kutambaza miguu juu anatakiwa ake sawa ashikwe
sawa sawa.