MAKUNDI
YA LESENI ZA UDEREVA NI YAPI?
Mfumo wa leseni za udereva
utakuwa na makundi mbalimbali ya madaraja ya leseni za udereva kama ifuatavyo:
Pikipiki
A – Leseni ya kuendesha pikipiki
zenye/zisizo na kigari na ambazo injini zake zina ukubwa zaidi ya cc 125 au
uzito wa kilo 230.
A1 - Leseni za kuendesha
pikipiki zisizo na kigari na ambazo ukubwa wake wa injini ni mdogo kuliko
cc 125 au chini ya kilo 230.
A2 – Leseni ya kuendesha pikipiki
za magurudumu matatu na manne.
A3 – Leseni za kuendesha pikipiki
baiskeli ambazo ukubwa wake wa injini hauzidi cc 50
Vyombo Binafsi vya Moto
B – Leseni ya kuendesha aina zote
za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki, magari ya biashara, magari makubwa na
magari ya kutoa huduma kwa umma.
Magari ya kutoa huduma kwa Umma
C – Leseni ya kuendesha magari ya
kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria 30 na zaidi pamoja na
dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo wa juu
unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na
leseni ya daraja CI au E kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
C1 – Leseni ya kuendesha magari
ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria 15 lakini wasiozidi 30,
abiria pamoja na dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo
wa juu unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa
na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
C- Leseni za kuendesha magari ya
kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria wanne lakini wasiozidi kumi
na tano. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo
unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na
leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
C3 – Leseni za kuendesha magari
ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria wanne au pungufu akiwemo
dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo
unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na
leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
Magari Madogo ya Mizigo ya
Biashara
D – Leseni ya kuendesha aina zote
za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki, magari makubwa na magari ya kutoa huduma
kwa umma.
Magari makubwa ya Mizigo ya
biashara
E – Leseni ya kuendesha aina zote
za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki na magari ya umma. Waombaji wanatakiwa
wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa muda usiopungua miaka mitatu.
Magari yenye Trela
F – Leseni ya kuendesha magari
yanayokokota trela.
Magari ya Shambani na Migodini
G – Leseni ya kuendesha magari ya
shambani na migodini.
Wanaojifunza
H – Leseni ya muda ya kujifunza
Kuomba leseni ya
udereva kwa mara ya kwanza
·
Uwe umehudhuria mafunzo katika Chuo chochote kinachofahamika na
kupewa cheti
·
Uwe na umri zaidi ya miaka 18 kwa ajili ya gari na umri wa miaka
16 na kuendelea kwa ajili ya pikipiki
·
Uwe na leseni ya kujifunzia/ya muda ya udereva
·
Uwe umelipa ada ya kufanyiwa majaribio - GRR
·
Uwe na cheti cha kupimwa macho
·
Uwe umepeleka maombi kwenye ofisi ya polisi wa usalama
barabarani kwa ajili ya kufanyiwa majaribio
·
Uende kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani ukiwa
na gari kwa ajili ya kufanyia majaribio
Baada ya mwombaji kufanyiwa majaribio anaweza kuruhusiwa
kuendesha pikipiki na magari madogo
Kubadilisha
leseni ya udereva (Daraja A B C D E F na G)
·
Mwombaji ataenda kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani
akiwa na leseni yake ya zamani ya udereva
·
lazima awe na cheti cha umahiri
·
mwombaji awe na umri zaidi ya miaka 18 kwa magari na miaka
16 kwa pikipiki
KUBADILI ILI KUPATA DARAJA ''C''
·
Mwombaji ataenda katika ofisi ya polisi wa usalama barabarani
akiwa na leseni yake ya zamani ya udereva
·
Awe na cheti cha umahiri
·
Mwombaji awe na umri zaidi ya miaka 18 kwa magari na miaka 16
kwa pikipiki
·
Cheti cha Gari la Kubeba Abiria (PCV) kutoka Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji au VETA
·
Mwombaji anatakiwa kubainisha aina ya gari analokusudia
kuendesha
·
Mwombaji atapewa daraja la leseni kulingana na mafanikio yake.
No comments:
Post a Comment